25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Karema wapata gari la kubebea wagonjwa

Na  Walter  Mguluchuma-Tanganyika.

 WAKAZI wa  Tarafa ya Karema  mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Tanganyika mkoani Katavi, wanaopakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wameondokana na tatizo la ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa lililokuwepo kwenye kituo chao cha afya cha Karema, baada ya Serikali kuwapatia  gari jipya.

Kabla ya kukabidhiwa gari hilo jana, wagonjwa wa  kituo hicho walilazimika kuagiza gari la wagonjwa  kutoka makao makuu yao ya Wilaya ya Tanganyika umbali wa kilometa 110.

 Gari  hilo lilikabidhiwa na Mbunge wa  Mpanda Vijijini, Moshi  Kakoso kwa uongozi wa halmashauri hiyo kutokana na maombi aliyotoa mwaka jana kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy  Mwalim.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,  Dk. Seleman Mtenjela  alisema   Serikali imefanya kazi kubwa ya  kujenga vituo viwili vipya na kukifanyia ukarabati kituo cha afya Karema, ujio wa gari hilo utasaidia utoaji huduma  uhakika kwa wagonjwa.

Alisema jukumu la Serikali, ni kuhakikisha watu wake wanakuwa  na afya njema hivyo tatizo la kituo hicho kuangiza gari kwenye makao makuu ya Halmashauri pindi anapokuwa ametokea mgonjwa anae takiwa kusafirishwa kwenda hospitali ya wilaya au ya mkoa sasa halitakuwepo tena .

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Salehe Mhando  alisema gari hilo halikupatikana hivi hivi, ni kutokana na jitihada za Kakoso kuomba Serikalini .

Diwani wa Kata ya Karema, Michael Kapata alisema ndoto za wakazi wa rarafa hiyo sasa zimetimia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles