NAIROBI, KENYAÂ
MATAIFA ya Afrika Mashariki ya Kenya na Uganda yanakabiliwa na tatizo la kitaifa la kukatika kwa umeme.
Kupitia mtandao wa Twitter, Shirika la Umeme la Kenya, Power and Lighting, limesema kuwa limepoteza uwezo wa kusambaza umeme kwenye gridi ya taifa kutokana na matatizo katika mfumo wake.
Katika taifa jirani la Uganda, hali ni kama hiyo hiyo baada ya shirika la kusambaza umeme, UETCL, pia kutangaza tatizo la kitaifa la kusambazwa kwa nguvu za umeme jana asubuhi.
Katika taarifa, kampuni ya Umeme Limited inayopata umeme wake kutoka kwa shirika la UETCL, imesema kuwa maofisa wa shirika hilo wanashughulikia tatizo hilo kuhakikisha limerekebishwa mara moja.
Bado haijabainika iwapo matatizo hayo katika mataifa hayo mawili yanaingiliana.