28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanyika, wenzake walalamika kukaa gerezani siku 526 bila upelelezi kukamilika

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Rais wa migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na wenzake wameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakilalamika kukaa gerezani siku 526 bila upelelezi kukamilika.

Washtakiwa hao waliwakilishwa jana na Wakili Hudson Ndusyepo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya wakati kesi hiyo il- ipokuwa ikitajwa kupitia mahakama mtandao.

Wakili wa Serikali Esther Mar- tine alidai kesi ilikuwa inatajwa, upelelezi haujakamilika wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Akijibu Wakili Ndusyepo al- idai barua iliandikwa na washtakiwa kwenda kwa mahakama wanalala- mikia upelelezi umechukua muda mrefu, sasa hivi zimefikia siku 526.

wanaomba mahakama imweleze DPP (Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali) aweze kujibu kiofisi kuhusu malalamiko yao ya upelelezi kuchelewa,”alidai.

Baada ya kusikiliza hoja hizo mahakama ilitoa amri kwa Wakili wa Serikali, awasiliane na mamlaka ya juu ili Mei 22 wakati kesi inakuja kutajwa waje na majibu.

Pia washtakiwa waliomba kuo- nana ana kwa ana na mawakili wao ili wajadiliane, maombi ambayo ya- likubaliwa ambapo mahakama im- eamuru Mei 22, washtakiwa waletwe mahakamani waweze kukutana na mawakili wao.

Mbali na Mwanyika washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo, Mkurugenzi Mtend- aji wa Pongea, North Mara na Buly- anhuku, Assa Mwaipopo, Kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washitakiwa hao wanakabiliwa

na mashtaka 39, yakiwemo ya utakat- ishaji na kukwepa kodi zaidi ya Dola za Marekani milioni 112.

Washtakiwa hao pia wanaka- biliwa na mashtaka matatu ya kula njama , mashtaka saba ya kughushi , mashtaka 17 ya utakatishaji wa fedha, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhali- fu wa kupangwa, mashtaka nane ya kukwepa kodi na shtaka moja la ku- toa rushwa.

Washtakiwa wanadaiwa, kutenda makosa hayo kati ya Aprili 11, mwaka 2008 na Juni 30, mwaka 2007 katika sehemu tofauti ya jiji la Dar es Sa- laam, Kahama mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maeneo mengine ambayo washtakiwa wanadaiwa kutenda ma- kosa hayo ni katika mji wa Johannes- burg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini Uingereza.

“Katika barua yao washtakiwa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles