30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Watoto wawili wa familia moja wafariki dunia baada ya kuangukiwa na nyumba

Na MALIMA LUBASHA -MUSOMA

MWANAMKE mmoja mkazi wa Mtaa wa Nyakato Mlimani, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Moshi Simon (29) amejeruhiwa vibaya huku watoto wake wawili wakifariki baada ya ukuta wa nyumba walimokuwa kuwaangukia.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, alisema nyumba hiyo ilianfuka kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha mkoani hapa na kusababisha mahafa hayo Mei 6 , saa 5.00 usiku.

Dk Naano aliwataja watoto waliofariki kuwa ni Joyce Malima (6) na mdogo wake Christopher Malima (3), ambao alisema walifariki baada ya ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala kuangukia kitandani.

Dk Naano alifika eneo la tukio na kuwaagiza viongozi wa Serikali
za mitaa kutembelea maeneo yao kubaini nyumba ambazo zipo mashakani kuanguka na kuwashauri wahusika kuhama maeneo hayo mara moja kuepuka madhara yana yoweza kutokea.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakato Mlimani, Malindo Jonas Mahamba, alisema wakati mvua inanyesha alipata
taarifa kwamba nyumba imeanguka na alifika eneo la tukio na kukuta mama na watoto wake wakiwa ndani.

Alisema aliomba msaada kwa majirani kuokoa familia hiyo kwa kuipeleka katika Kituo cha Afya Nyasho ambapo mtoto wa miaka 6 alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu huku
mdogo wake akipelekwa Hospitali Rufaa ya Musoma ambaye naye umauti ulimfika akiwa anapatiwa matibabu.

Mahamba alisema nyumba nyingi za mtaa wake zimejengwa kwa matofali mabichi ambazo siyo imara na kushauri wananchi kuondoka maeneo hayo na kuhamia sehemu salama zaidi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles