25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi walalamikia polisi K’njaro

Na Upendo Mosha,Moshi

WANANCHI mkoani Kilimanjaro, walitupia lawama jeshi la polisi mkoani humo kwa kushindwa kudhibiti wimbi la uporoaji wa kutumia silaha na mauaji.

Hatua hiyo, imekuwa siku chacha tu,baada ya mauaji ya mfanyabishara maarufu mjini Moshi, Josephat Mahalo (36) maarufu kwa jina la Tajiri mtoto.

Wakizungumza na MTANZANIA  kwa nyakati tofauti  juzi mjini Moshi,wamesema matukio ya uhalifu yameendelea kushika kasi maeneo mbalimbali ya mkoa  huo tofauti na miaka ya hivi karibuni.

Walisema jeshi la polisi, limekuwa likiyafumbia macho,japo wanadai mauaji hayo yamekuwa yakitokea kutokana na ulipizaji wa visasi jambo ambalo si sahihi.

Mmoja wa wananchi hao, Ernest Ndensau, alisema katika kipindi cha miezi minne mfululizo, matukio ya uhalifu wa kutumia silaha yamekithiri maeneo mengi.

“Jeshi la polisi linawajibu mkubwa wa kuhakikisha linakisaka kikundi cha majambazi kinachomiliki bunduki aina ya Shortgun…kimekuwa kikinafanya uhalifu kwa miezi minne mfululizo.

“Bahati mbaya polisi hawajaonyesha dhamiri ya kukomesha tatizo hili,”alisema Ndenshau.

Alisema haamini kama polisi wameshindwa kukipata kikundi hicho kinachoendelea kusumbua wakazi wa mji wa Moshi pamoja na intelejensia wanayojisifu kuwa nayo katika  kubaini matukio ya uhalifu.

Naye Florah Mlay, alisema polisi wanapaswa kufanyika taarifa wanazopewa, badala ya kusema matukio hayo yanahusishwa na ulipizaji wa kisasi jambo ambalo halina ukweli wowote.

“Siku kama tano sasa zilizopita, tumeshuhudia mauaji ya mfanyabiashara mkubwa hapa Moshi, polisi wanadai ni ulipizaji wa kisasi kisa tu, alikutwa na mitambo na vifungashio  vya pombe kali aina ya Konyagi, lazima polisi wa watafute wauaji na bastola ya marehemu ambayo waliondoka nayo,”alisema

Alisema bastola iliyoporwa na waalifu hao, baada ya kufanya tukio hilo, itaendelea kutumika katika matukio mengine ya uhalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Flugence Ngonyani alipotafutwa kujibu malalamiko hayo, simu yake ya kiganjani iliita muda mrefu bila kupokelewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles