26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ulimwengu ahusishwa kutua Ufaransa

thomas-ulimwenguNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

NYOTA ya mshambuliaji wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Thomas Ulimwengu, imezidi kung’ara baada ya kupata dili lingine barani Ulaya.

Klabu ya TP Mazembe imethibitisha kupokea ofa kutoka klabu ya AS Sainti Etienne inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 na huenda straika huyo akaungana na Mbwana Samatta kucheza soka la kulipwa barani Ulaya baada ya taarifa za mshambuliaji huyu kukaribia kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji.

Awali kabla ya ofa hii mpya, Ulimwengu alihusishwa na timu ya Besiktas ya Uturuki lakini baadaye mambo yakabadilika ambapo sasa uongozi wa TP Mazembe umesema upo tayari kumruhusu Ulimwengu kwenda kukipiga nchini Ufaransa.

Timu ya AS Saint-Etienne inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligue 1 baada ya kucheza mechi 19 ambapo imejikusanyia pointi 29, ikishinda mara tisa, kufungwa mechi nane na kupata sare mbili.

Inasemekana TP Mazembe wamefikia uamuzi wa kumwachia mshambuliaji huyo ambaye nyota yake ilianza kung’ara tangu ajiunge na klabu hiyo ili kumwondoa katika hali ya upweke anayoweza kubaki nayo atakapoondoka Samatta ambaye waliishi kama mapacha.

Mabingwa hao wa Afrika wameona ni vyema Ulimwengu naye aondoke ili akajiunge na klabu mpya ambayo atakutana na changamoto mpya kuliko kuendelea kuichezea timu hiyo bila ya pacha wake Samatta ambaye muda wowote anatarajiwa kuanza kibarua chake katika klabu ya KRC Genk.

Kwa sasa Samatta ambaye ni mmoja wa wafungaji bora kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka uliopita, anasubiri kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika ambayo ameingia katika tatu bora.

Mafanikio ya kucheza soka barani Ulaya kwa nyota hao ambao wanaichezea timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, yataweza kukisaidia kikosi hicho pamoja na kutoa fursa kwa wachezaji wengine wa Tanzania wenye ndoto za kucheza Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles