MSANII wa muziki wa RnB nchini, Benald Paul ‘Ben Pol’, amepanga kuwafanyia ‘surprise’ mashabiki wake mwanzoni mwa mwaka 2016 kwa wimbo mpya alioufanya na msanii mkubwa kutoka Afrika Mashariki.
Akizungumza na MTANZANIA jana, mwanamuziki huyo alisema amemaliza mwaka kwa wimbo mpya na atafungua mwaka kwa wimbo mpya.
“Nimefunga mwaka kwa kuachia video yangu mpya ambayo inajulikana kwa jina la ‘Ningefanyaje’ huku nikishirikiana na Avril kutoka Kenya, ila nitafungua mwaka kwa wimbo mpya ambao sitapenda kuutaja jina mapema, lakini nimefanya na msanii toka nje ya Tanzania na itakuwa ni ‘surprise’ kwa mashabiki wangu,” alisema Ben Pol.
Msanii huyo aliongeza kwa kusema kwamba, mwaka 2016 utakuwa wa mafanikio makubwa kwake kutokana na jinsi alivyojipanga na ushindani uliopo.