Leonard Mang’oha, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemshauri Rais Dk. John Magufuli kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ikiwamo Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Profesa Lipumba metoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 10, katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine pia amemshauri kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ili kuviruhusu vyama kueneza sera zake kwa wananchi.
“Sheria ya vyama vya siasa inataka kila chama kuwa na rejesta, lakini utekelezaji wa kipengele hicho unahitaji kuhamasisha wananchi.
“Kwa hiyo tunapohitaji mikutano ya hadhara si tu kueneza sera, pia tunataka kutekeleza mara kwa ya Sheria ya vyama vya siasa,” amesema Profesa Lipumba.
Amesema mchakato wa ukandamizaji demokrasia utafanikiwa ikiwa wananchi wakiwa wakiwamo wanachama wa chama hicho kutaja kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hata kama mazingira hayaruhusu kufanya hivyo.
Kuhusu CUF kusimamisha wagombea, amesema Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho limeshaamua kuwa litasimamisha wagombea katika ngazi zote Tanzania Baraza na Visiwani.
Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuielewa vema sheria ya vyama vya siasa na kuacha kuvizuia vyama vya upinzani kutekeleza haki yake ya kisheria ya kufanya mikutano.