25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mbagala yafurika wahitaji wa vyeti kuzaliwa

Na Asha Bani-Dar es salaam

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA ) umepiga kambi katika viwanja vya Mbagala Zakhem kkwaajili ya zoezi la kusajili wananchi ili wapate vyeti vya kuzaliwa.

Zoezi hilo litarahisisha pia wananchi kuwa na taarifa za upatikanaji wa cheti cha kupigia kura cha NIDA.

Kwa mujibu wa Meneja Masoko na Mawasiliano RITA Josephat Kimaro alisema alisema lengo la zoezi hilo ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za wakala hivyo kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo mbalimbali.

” Kwa siku za karibuni mahitaji ya cheti cha kuzaliwa yameongezeka sana katika maeneo yote ya nchi ikichangiwa zaidi na wananchi wanaohitaji cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya kupata Kitambulisho cha Taifa watakachokitumia kusajili line za simu kwa alama za vidole,”

” Kutokana na ongezeko hilo RITA imefanya juhudi mbalimbali kukabiliana na ongezeko la wananchi ikiwa pamoja na kuanzisha vituo vya huduma nje ya ofisi,”alieleza Kimaro.

Alisema kwa    zaidi ya miezi miwili RITA imekuwa na kituo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambacho kimekuwa kikisajili wastani wa watu 600 kwa siku.

Alisema kwa zoezi la usajili katika Viwanja vya Zakhiem ni sehemu ya Tamasha la Maisha ni kidole ambalo limeandaliwa na Kituo cha habari cha EFM lililo na.lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usajili kwa njia alama za vidole ambalo pia limeshirikisha wadau wengine kama NIDA, Mamlaka ya Mawasiliani nchini (TCRA) na makampuni yote ya Simu.

Aliongeza kuwa katika banda la RITA mpaka sasa zaidi ya fomu za maombi 1000 zimekwishagaiwa na wananchi wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha ili wapate vyeti vyao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles