27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC SABAYA AAGIZA WAMILIKI WA MABASI WAJISALIMISHE POLISI

Na Omari Mlekwa, Hai

MKUU wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataka wafanyabiashara  wawili  wa mabasi ya Machame Safari na Limu safari kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Bomang’ombe kutoka na kuwepo kwa taarifa za kuhujumu miundombinu ya reli.

Wafanyabiashara hao waliotakiwa kuripoti kituo cha Polisi Bomang’ombe leo  Jumapili Januari 19, 2020 kabla ya saa 10 jioni ambao Clemence Mbowe anayemiliki mabasi ya Machame Safari na Rodrick Uronu anayemiliki mabasi ya Lim Safari

Wamiliki hao kwa pamoja wanatuhumiwa  kuunda genge la uhalifu kwa lengo la kuhujumu miundombinu ya reli ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam- Moshi.

Sabaya alitoa agizo hilo baada ya kutembelea ukarabati wa ujenzi wa eeli katika kijiji cha Rundugai ambapo alisema kuwa kumekuwepo na taarifa za kuhujumu miundombinu ya Reli ambao unaendele kuelekea mkoani Arusha

“Nimepata taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wawili wana genge la kuhujumu ujenzi huu ili kukwamisha juhudi za serikali za kurahishia wananchi usafiri na kuwapunguzia adha ya usafiri,” amesema Sabaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles