31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Kabendera yasogezwa hadi mwakani

Mwandishi wetu-Dar es Salaam.

MWANDISHI wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, sasa atalazimika kukaa gerezani wakati wote wa sikukuu hadi Januri kesi yake itakapotajwa tena.

 Kabendera ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, jana alifikishwa mahakamani kwaajili ya kesi yake kutwajwa huku baadhi ya maofisa wa balozi za Uingereza na Marekani wakihudhuria kuisikiliza.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega, alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado unaendelea, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa,” alidai wakili Simon.

Baada ya Simon kueleza hayo, Jebra Kambole ambaye ni Wakili wa Kabendera, aliomba  upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi kwa wakati ili kesi hiyo iweze kuendelea.

Alidai bado wanaendelea na mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) kuhusu barua ya kukiri na kuomba msamaha aliyoiandika Kabendera kwenda kwa DPP.

“Kesi hii ilivyoahirishwa wiki mbili zilizopita mahakama ilituambia tufuatilie kwa DPP kujua mazungumzo yamefikia hatua gani, naomba niseme tu tumeshafanya hivyo na mazungumzo bado yanaendelea.

” Tutaifahamisha mahakama hii kadri mazungumzo yatakavyokuwa yanaendelea” alidai Kambole.

Hakimu Mtega baada ya kusikiliza hoja za pande zote, alihirisha kesi hiyo hadi Januari 2, 2020 itakapotajwa tena.

Mshtakiwa alirudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Kabendera alifikishwa  Kisutu kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles