27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Amshambulia mkewe kwa kuchinja jogoo la Krismasi

BUDAKA, UGANDA

MWANAUME mmoja mwenye umri wa miaka 50 kutoka Wilaya ya Budaka mashariki mwa Uganda, amemjeruhi mke wake vibaya baada ya mwanamke huyo kumchinja kuku aliyetakiwa kufanywa kitoweo wakati wa sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, bwana huyo alimnunua kuku kwa Sh 15,000 za Uganda takribani shilingi za kitanzania 9400 akipanga kumchinja siku ya Krismasi, lakini kwa bahati mbaya mke wake aliamua kumchinja na kumuandaa siku ya Jumapili Disemba 15.

Kwa mujibu wa katibu wa habari wa eneo hilo, Joseph Gadimba, baada ya mume kugundua kuwa kuku huyo hayupo tena, alimpiga mke wake na kumlaumu kwanini amemchinja bila ruhusa yake.

Bw Gadimba amesema; ”alimpiga na kumchapa mke wake mara nyingi, huku akimuacha akipigania uhai wake.

Kwasasa mwanamke huyo anatibiwa katika Kituo cha Afya cha Budaka, mashariki mwa Uganda.

Wakazi wa eneo hilo walimtaka mwanaume huyo achukue majukuu yote yanayohusu matibabu ya mkewe ambayo alikubali kugharamia na kesi hiyo kutoripotiwa polisi.

”Pale mwanamke huyo atakapo pona, ndugu zake kutoka eneo la Kapyani-Kasasira katika wilaya ya Kibuku, wanatarajia kufanya kikao na mwanaume huyo kujua chanzo cha yeye kumpiga mtoto wao na kutatua kesi hiyo,” alisema Gadimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,894FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles