32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kodi ya TRA yazua kizaazaa Bakwata

Sheikh-Abubakar-Zuberi-bin-AllyNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MUFTI na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi, ameunda timu ya uchunguzi ambayo itapitia upya mikataba yote mibovu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Pamoja na hali hiyo pia ametangaza kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Utawala wa Bakwata, Makao Makuu,  Karim Majaliwa   kupisha uchunguzi juu ya kadhia ya magari 82  na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mufti Zuberi ilieleza kuwa hatua hiyo ni ya kulifanyika maboresho baraza hilo.

“Nimeunda timu ya uchunguzi ambayo nimeipa pia majukumu ya kupitia mikataba yote ya Bakwata   kuangalia   mikataba mibovu na kuona namna ya kufanya  iweze kuwa na mikataba yenye masilahi na Bakwata kwa niaba ya Waislamu.

“Timu hii nimeipa majukumu ya kukagua hesabu za BAKWATA kuanzia   makao makuu na nchi nzima. Na kwa mamlaka niliyonayo, nimemsimamisha kazi Karim Majaliwa – Mkurugenzi wa Utawala wa BAKWATA Makao Makuu,   kupisha uchunguzi juu ya kadhia ya magari 82  na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi,” alisema Mufti Zuberi katika taarifa yake.

Licha ya hatua hiyo, Mufti Zuberi  aliwataka Waislamu nchini kutambua kuwa baada ya siku chache Waislamu watakuwa wameingia katika Mwezi wa Mfungo sita.

“Waislamu wote duniani unapofika mwezi wa mfungo sita husherehekea juu ya mazazi ya Mtume S.A.W. Baraza kuu la Waislamu wa Tanzania linapenda kuwafahamisha juu ya utaratibu wa matukio tuliyoyapanga katika kipindi hiki cha mwezi wa kuzaliwa  kwa Mtume.

“Katika wiki ya kwanza ya mwezi huu wa mfungo sita kutakuwa na wiki ya misikiti… ndani ya wiki hii waislamu watatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika majukumu yao ya kila siku ya kuhakikisha   mazingira yao yote yanakuwa katika usafi wa hali ya juu kama ilivyo kawaida,” alisema.

Aliwataka masheikh na maimamu nchi nzima kutumia kipindi  cha mwezi wa kuzaliwa kwa Mtume S.AW  kumuelezea kwa kina katika nyanja mbalimbali kama vile elimu, siasa, uchumi, uongozi na utawala bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles