27.7 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 80 ya udongo wa Tanzania unahitaji mbolea ya Minjingu

Na Mwandishi Wetu

TAKRIBANI asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima. Shughuli hiyo ndiyo inawaingizia kipato ili waweze kukidhi mahitaji yao muhimu, ikiwamo kusomesha watoto wao, kugharamia matibabu na kadhalika.

Hata hivyo, wengi wamejikuta wakiishia kupata mazao yanayowatosha kwa chakula tu – bila ziada, huku wengine wakiishia kutupa nguvu na muda wao bure.

Hali hiyo inatokea licha ya kulima eneo kubwa la ardhi ambalo kimsingi lingepaswa liwapatie chakula cha kutosheleza mahitaji yao katika familia pamoja na kupata ziada ambayo kama ingeuzwa ingewasaidia kwa mahitaji mengine muhimu.

Mkurugenzi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu(Minjingu Mines and Fertilizer Ltd – MMFL) , Pardeep Singh Hans ‘Tosky’, akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa, alipotembelea kiwanda cha Minjingu Novemba, 2017 wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Ama kwa hakika wakulima hawa, wengi walikuwa hawajui sababu za kutopata mazao mengi na bora.

Hata hivyo utafiti wa viwango vya asidi, alkali na afya ya udongo uliofanywa hivi karibuni nchini umeainisha msingi wa tatizo hilo.

Kwa mujibu wa utafiti huo, eneo kubwa la udogo nchini una kiwango kikubwa cha asidi ambacho kinahitaji mbolea ili kuweza kupata mazao bora na kwa wingi.

Utafiti huo umetoa mwanga kwamba suluhisho la wakulima ni kutumia mbolea ya Minjingu kama wanahitaji kuepuka tatizo la kulima eneo kubwa na kupata mazao ambayo hayawatoshelezi hata kwa mahitaji ya chakula.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd – MMFL) Pardeep Singh Hans ‘Tosky’, anasema mbolea ya Minjingu ina uwiano sawa wa virutubisho katika kila punje na imeonekana kufanya vizuri na kuwanufaisha wakulima wengi hapa nchini.

Tosky anasema kutokana na utafiti wa viwango vya asidi na alkali na afya ya udongo Tanzania, mbolea ya Minjingu inafaa katika eneo la asilimia 80.3 ya ardhi inayolimwa mazao mbalimbali.

 “Hii inadhihirisha kwamba mbolea ya Minjingu inafaa kwa matumizi ya udongo kwa karibu nchi nzima,” anasema Tosky.

Anasema kwa sasa asilimia 90, mbolea zinazotumika hapa nchini huagizwa kutoka nje ya nchi.

 “Mbolea hizo huletwa zikiwa zimewekwa viwango vya virutubisho ambavyo si rahisi sana kuvibadilisha ili viendane na mahitaji ya mimea pamoja na hali ya udongo kwa kuzingatia afya ya udongo wa Tanzania,” anasema Tosky.

Pamoja na hali hiyo, anasema mbolea ya Minjingu inafaa katika uzalishaji wa mazao mengi hapa nchini, hivyo wakulima wanapaswa kuitumia kwa wingi kwa kuwa inatumika kuzalisha mazao mbalimbali.

 “Kati ya mikoa yote ya Tanzania Bara, ni michache ambayo mbolea ya Minjingu huhitajika kwa kiwango kidogo, hususan kwenye maeneo ya kilimo cha umwagiliaji. Mikoa hiyo ni pamoja na Arusha, Kilimanjaro, Simiyu na Shinyanga,” anasema.

Pia anasema kwa muda mrefu sasa, wakulima wengi katika mikoa mashuhuri ya uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini wamejenga mazoea ya kutumia mbolea za aina moja kwa kipindi kirefu zilizopendekezwa miaka mingi iliyopita.

 “Mazoea ya matumizi ya mbolea hizo kwa muda mrefu, hususan mbolea za DAP, Urea, SA na CAN yanaendelea kusababisha tija ndogo na uzalishaji hafifu wa mazao kwa wakulima.

 “Hii ni kwa sababu virutubisho vya mbolea hizo havitumiki kama inavyotarajiwa kwa ajili ya mimea inayooteshwa katika udongo wenye asidi kali na asidi ya wastani.

 “Maeneo haya yanaonyesha kuwa na upungufu wa kirutubisho cha naitrojeni (N), fosiferasi (P), potasiamu (K), salfa (S), kalshiamu (Ca) na magnesiamu (Mg).

“Aidha, udongo wa maeneo haya umeonekana kuwa na kiwango kikubwa cha chuma (Fe), manganizi (Mn) na pengine boroni (B).

“Ili kuondokana na kadhia hii, wakulima katika maeneo hayo ya uzalishaji wanashauriwa kutumia chokaa (lime) na mbolea zisizo na asidi zilizosheheni virutubisho vya N, P, K, S, Ca na Mg.

“Kutokana na hali hiyo, tunashauri wakulima wabadilike kwa kuzingatia ushauri wa kilimo cha kisasa chenye kuzingatia mahitaji halisi ya virutubisho muhimu kwenye udongo na hatimaye kwa ajili ya mimea,” anasema Tosky.

Kwa mujibu wa Tosky, katika kuleta mafanikio kwa wakulima, Minjingu Mines and Fertilizer Ltd ina mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu.

Anasema kwa mipango ya muda mfupi ni pamoja na kutoa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea zinazozalishwa hapa nchini kwa kuzingatia hali ya afya ya udongo.

 “Jambo hili litaenda sambamba na matokeo ya upimaji wa hali ya afya ya udongo na kuongeza virutubisho muhimu vinavyotakiwa na mimea.

Tumbaku ilivyostawi kutokana na matumizi ya mbolea ya Minjingu

 “Hii ni kwa sababu mbolea nyingi zinazoingizwa nchini zina virutubisho vikuu vya kwanza bila kuwepo kwa virutubisho vya upili na virutubisho vidogo ambavyo vinachangia kwa kasi kikubwa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo,” anasema Tosky.

Anasema katika mpango wa muda wa kati, ni kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea za kutosha hapa nchini kwa madhumuni ya kukidhi mahitaji ya wakulima kulingana na hali ya afya ya udongo.

“Kwa mfano, mahitaji halisi ya mbolea nchini ni tani 586,000 kwa mwaka 2019/20. Kiwango hiki cha uzalishaji kinaweza kufikiwa endapo wakulima watakuwa na mwamko thabiti wa matumizi ya mbolea na kuongeza uzalishaji wa mbolea katika Kiwanda cha MMFL.

“Aidha, katika mipango ya muda mrefu ni kuhakikisha kuwepo kwa uzalishaji endelevu wa mbolea za aina zote kwa ajili ya wakulima wa Tanzania na Ukanda wa Afrika ya Masharik na Kati.

“Hii ni kwa sababu tunayo rasilimali za kutosha kuanzia wataalamu, malighafi na uwezo wa kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea.

 “Uzalishaji huo unatakiwa kuzingatia mahitaji halisi, ufungaji wa mitambo mipya ya kuchimba, kuchakata na kutengeneza mbolea zenye kulenga kuleta matokeo chanya kwa wakulima na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” anasema Tosky.

NCHI JIRANI WANAIHUSUDU MBOLEA YA MINJINGU

Kwa sasa mbolea za Minjingu zimefahamika sana katika soko la nje ya Tanzania, hususan nchini Kenya, Rwanda na Burundi.

“Hii inatokana na mwamko wa wakulima na uwezo wa kubadilika kimawazo kuhusu faida ya kutumia mbolea zenye viwango vya ubora kulingana na afya ya udongo wa maeneo husika.  “Kwa sasa, Serikali za nchi hizo pamoja na wakulima wanazingatia uwepo wa virutubisho vikuu vya kwanza, vya upili na vidogo kwa wakati mmoja katika udongo kwa manufaa ya mimea inayozalishwa,” anasema Tosky.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles