Na GLORY MLAY
STAA wa Bongo Fleva, Lameck Jacob ‘Bonge la Nyau’, amesema anafuata nyayo za wakongwe Alikiba na Dully Sykes kwa kutochora michoro ya mwilini maarufu kama tattoo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Bonge la Nyau anayetamba na wimbo wake mpya Kitochi, alisema anapenda kujulikana kutokana na kazi zake na siyo kuchora tattoo na kutoboa masikio kama wanavyofanya mastaa wengine.
“Ali na Dully wanaimba vizuri na kazi zao zinatambulika hafanyi vibaya eti kisa hajatoboa masikio au hajachora tattoo, naamnini usafi unaanzia kwenye mwili,” alisema Bonge la Nyau.