31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Baada ya hasara ya mamilioni Kenya yazindua reli nyingine ya SGR kupunguza msongamano

NAIROBI, KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua mradi wa reli ya kisasa maarufu SGR utakaounganisha uwanja wa Kimataifa wa Jommo Kenyatta hadi jijini Nairobi. 

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu itolewe taarifa iliyoonyesha  kwamba   Kenya imepata hasara ya dola milioni moja katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa reli yake nyingine ya  kisasa kutoka Nairobi kwenda Mombasa, ijulikanayo kama SGR.

Serikali ya China imeijenga reli hiyo kwa mkopo wa dola bilioni 3, utakaolipwa kwa kipindi cha miaka 15 ijayo. 

Wakati hali ikiwa hivyo, Reli aliyozindua jana ambayo itagharimu  dola milioni sita inatajwa kuwa itapunguza msongamano mkubwa wa magari. 

Mradi huo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Nairobi, ambalo idadi ya watumiaji wa magari inazidi kuongezeka.

Benki ya Dunia (WB) ilikisia kuwa taifa  hilo hupoteza takribani dola 5,000 kila siku kutokana na misongamano ya magari huku watu wakipoteza muda wao kwenye misongamano hiyo.

Msongamano wa magari pia huchangia wasafiri kukosa safari zao za ndege katika uwanja huo wa kimataifa wa Jommo Kenyatta. 

Rais Uhuru Kenyatta alisema amezindua mradi huo baada ya Benki ya Dunia kujiondoa kwenye ubia na serikali ya Kenya. 

“Wengine wanasema ooh! hii reli inaenda wapi? hakuna kitu kibaya kama ujinga wa mtu ambaye fikra zake ni namna hii. Sasa sisi tukisema tunajenga hii kusaidia wananchi tatizo iko wapi?”, alisema Kenyatta. 

Mradi huu ni matokeo ya ziara ya Rais Kenyatta mwezi Septemba mwaka jana katika taifa la China, kwenye kongamano lililowaleta pamoja viongozi wa Afrika pamoja na wawekezaji.

Mradi huu utatekelezwa na kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China, kwa ushirikiano na Serikali ya Kenya na mashirika ya binafsi.

Inakadirikwa kuwa magari elfu 60 hutumia barabara hiyo kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jommo Kenyatta hadi Westlands kila siku.

Aidha mradi wa barabara unaotekelezwa nao ukikamilika idadi ya watumiaji magari itaongezeka kwa magari 25,000. 

Barabara  hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 17. 

Badala ya kuchukua saa nyingi kufika uwanja wa kimataifa, barabara hiyo itakapokamilika mtumiaji atatumia dakika 10 au 15 kutoka katikakati ya jiji.

Hata hivyo wataalam wanasema kuwa mradi huo ni ghali mno ikilinganishwa na gharama inayostahili kuchukuliwa huku ushirikiano kati ya China na Afrika ukiendelea kupanuka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles