26 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 2,500 huzaliwa na midomo sungura nchini kwa mwaka

AVELINE KITOMARY NA BRIGITHER MASAKI-DAR ES SALAAM

WAKATI juzi dunia ikiadhimisha siku ya mdomo wazi (sungura), imeelezwa kuwa nchini watoto  2,500  huzaliwa wakiwa na  tatizo la mdomo wazi kila mwaka .

Tafiti zinaonyesha kati ya watoto 700 wanaozaliwa duniani kote mmoja huzaliwa na tatizo hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika maadhimisho hayo, Daktari wa  mifupa na upasuaji kutoka Hospitali ya CCBRT, Dk. Zainab Illonga,  alisema   pamoja na tafiti hizo kutokuonyesha chanzo cha watoto kuzaliwa na midomo wazi, tatizo hilo hutokea wakati mimba ikiendelea kukua.

Dk Illonga alisema mama mjamzito mwenye ugonjwa wa kisukari, anayevuta sigara, mwenye unene uliopitiliza yuko kwenye hatari zaidi ya kupata mtoto mwenye ndomo wazi.

“Kipindi cha mwanzo cha mimba na ukuaji wa mtoto akiwa tumboni mdomo wa ndani na wa nje huwa inajikunja na kukutana pamoja, wakati mwingine ikishindikana kujikunja ndio mtoto huzaliwa na mdomo wazi,”alisema Dk Illonga.

Awali Mkurugenzi wa  Shirika lisilo la kiserikali la Smile Train, Jane Ngige, alisema jukumu lao ni kusaidia watoto hao kupatiwa huduma za upasiaji bure.

Alisema tangu mwaka 1999 wameweza kuwasaidia watoto zaidi ya milioni 1.5 kurudishiwa tabasamu lao na kwa watu wenye midomo wazi.

 “Hadi sasa  tumeweza kuwasaidia watoto zaidi ya 3,000 katika hospitali ya CCBRT, watoto hufanyiwa upasuaji bure. Tunashirikiana na hospitali ili kuhakikisha huduma ya upasuaji inatolewa bure,”alisena Jane.

Alisema kwa Tanzania shirika hilo linashirikiana na hospitali nane kwa lengo la kuhakikisha  wabawarudishia tabasamu watoto hao.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wenye matatizo ya mdomo wazi katika hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles