BAADHI ya watoto wa wanamuziki wa zamani wameibuka na kudai kwamba wamesikitishwa na mitandao mbalimbali inayouza nyimbo za wazazi wao bila kuwa na makubaliano na familia zao.
Mmoja wa watoto hao akimwakilisha msanii Kassim Njohole aliyekuwa akipiga katika bendi ya ‘Njohole Jazz Band’, Hassan Kassim Njohole maarufu ‘Hanjo Hassan, aliliambia MTANZANIA kwamba familia zao zinashangazwa kuona mitandano ya ndani na nje ya nchi ikiuza nyimbo za wazazi wao bila familia kupata faida yoyote hata ya kushirikishwa katika makubaliano ya kuuza nyimbo hizo.
Hassan aliongeza kwamba familia yao imeshaanza kuchukua hatua za awali za kufuatilia mitandao ya ndani na nje inayouza nyimbo hizo ili wafahamu kiundani sababu za kuuza kazi hizo bila familia yake kunufaika nazo.
“Nimesafiri kutoka Morogoro mpaka Dar es Salaam ili kufahamu ukweli juu ya mitandao hiyo ambayo mingine ipo Kenya.
Mwanamuziki Njohole aliwahi kuwika miaka ya 60 akiwa na nyimbo za uhuru, ukiwemo wimbo wa ‘Dada pili’ alioutoa mwaka 1964.