22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Priscilla Samweli ndiye Miss Albino Kanda ya Dar es Salaam

MISS ALBINONA GEORGE KAYALA

MREMBO kutoka Chanika, Priscilla Samweli (22) aliyenyakua taji la Miss Albino 2015 Kanda ya Dar es Salaam, juzi amekuwa mshiriki wa kwanza kusubiri washindi wengine watakaoshindanishwa katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Albino Tanzania.

Mratibu wa shindano hilo, Alexander Matowo, alisema shindano hilo linalofanyika kikanda, awamu ya kwanza imeanza kanda ya Dar es Salaam na Priscilla ameibuka mshindi, hivyo atapambanishwa na warembo wengine watakaopatikana katika kanda nyingine zitakazotajwa siku zijazo ili kumpata Miss Albino Tanzania.

Shindano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Msasani Club, ambapo Priscilla aliibuka na Sh 300,000, huku mshindi wa pili, Lilian Msime akiondoka na kitita cha Sh 200,000 na mshindi wa tatu, Ratifa Abdul akishika nafasi ya tatu na kupata Sh 100,000.

“Wasichana wenye ulemavu wa ngozi tumekuwa tukibaguliwa katika harakati mbalimbali, lakini tunashukuru shirika hili limetukutanisha nami nimeibuka mshindi, hivyo naomba wasichana wengine katika kanda nyingine wajitokeze kwa wingi ili kushiriki shindano hili na hatimaye tumpate Miss Albino Tanzania,’’ alisema Pricilla.
Shindano hilo liliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation (SVF).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles