Ferdinanda Mbamila, Dar es Salaam
Idara ya mafunzo kupitia mafunzo ya financial freedom (CITL), wameandaa bonanza kwa lengo la kuwakutanisha vijana kwa kutumia michezo mbali mbali ili kuwahamasisha na kutambua fursa mbali mbali zinazotokana na masoko makubwa duniani.
Akizungumza jijini dar es salaam Mkuu wa idara ya mafunzo CITL Nicholaus Mwakyonde amesema, bonanza litaanza tarehe 28 mwezi wa tisa katika vijawanja vya ustawai wa jamii kuanzia asubuhi likiwa na lengo la kuwakutanisha vijana na masoko makubwa duniani ikiwemo soko la hisa, masoko ya forex, , masoko ya bidhaa duniani na masoko ya vito duniani.
Nicholaus amesema bado kuna changamoto kubwa ya elimu kwa vijana juu ya namna ya kutunza fedha na matumizi sahihi ya fedha, hivyo wameamua kuwafundisha vijana namna ya kutafuta vipato na matumizi yake sahihi kwa kutumia bonanza.