25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

DED alia ukatili kushamiri Hanang

Mohamed Hamad – Hanang

VITENDO vya kikatili vinavyoendelea katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, vinatakiwa vitafutiwe ufumbuzi ili wananchi waondokane na madhara yanayoendelea kujitokeza kila kukicha.

Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Bryceson Kibasa, alipokuwa akizungumza na Kamati ya Wasaidizi wa Kisheria  katika mafunzo yaliyoandaliwa na Asasi ya Haliso kwa kushirikiana na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.

Alisema anaamini mabadiliko hayo yatatokana na kupatikana elimu kwa jamii.

“Nilipofika miaka mitatu iliyopita hapa, niliambiwa huko ni eneo la wafugaji hawapendi elimu, nataka kuwahakikishia kuwa sio kweli, mwamko wa wazazi kwa sasa ni mkubwa sana, tumejipanga kuwa hata wanaokuja na taarifa za matokeo mabovu shuleni na kueleza sababu kuwa ni mwamko mdogo tunakataa na kushauri zifutwe,” alisema Kibasa.

Alisema kuna vitendo vinavyojitokeza kwa baadhi ya wazazi kufanya makubaliano watoto wao kwenda kufanya kazi za ndani mijini na kuacha haki zao za kupata elimu na kutaka hata vitendo vya ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike tena wakiwa wadogo vikome.

Mratibu wa Uwezeshaji Jamii Kisheria, Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Consolata Chikoti, alisema ili kamati hiyo iwe na mafanikio, jamii inatakiwa kutoa ushirikiano, wasiwaone maadui, wajue kuwa wana nia njema ya kusaidia jamii.

“Tumeamua kuja Hanang na kutoa mafunzo hayo kwa sasabu tumeona hii jamii ina uhitaji wa aina yake, ina watoto wenye vipaji, lakini kuna vikwazo vikiwemo mila na desturi kandamizi kwa watoto wa kike na wanawake na sasa takwimu za ukeketaji katika Mkoa wa Manyara ni asilimia 58,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles