Tehran, iran
RAIS Hassan Rouhani ameitaka Marekani iondoe kwanza vikwazo vyote dhidi ya nchi yake, siku moja baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kusema yuko tayari kwa mazungumzo.
Katika hotuba yake iliyotangazwa moja kwa kupitia televisheni, Rouhani alisema funguo za mabadiliko chanya ziko mikononi mwa Washington, kwa sababu Iran tayari ilishaondoa uwezekano wa kufanya jambo linaloitia wasiwasi zaidi Marekani – ambalo ni kutengezena bomu la nyuklia.
Rais Emmaneul Macron wa Ufaransa alisema jana kuwa maandalizi yanafanyika kwa mkutano kati ya Trump na Rouhani katika wiki zijazo, ili kutafuta suluhisho la mkwamo wa nyuklia.
Mei mwaka jana, Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, na kisha ikarejesha vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Iran.