28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Japan kujadili msaada kwa Afrika

Tokyo, japan

JAPAN itakuwa mwenyeji wa mkutano wa maendeleo na viongozi wa Afrika wiki hii, ikitazamia kuimarisha uwepo wake barani humo.

Nchi hiyo ya Asia pia inatarajia kutoa mapendekezo mbadala kwa uwekezaji wa China inayozidi kujiimarisha barani Afrika.

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, alisema anataka duru hii ya mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika – TICAD, kusaidia kuzindua mkakati wake wenye athari barani humo.

 Na mkutano huo unaofanyika karibu kila miaka mitano tangu 1993 nchini Japan au katika nchi ya Afrika, unakuja wakati kuna ongezeko la uwekezaji kutoka China, ambayo ilitangaza kiasi cha dola bilioni 60 katika ufadhili wa maendeleo ya Afrika mwaka jana.

 Kiasi hicho ni mara mbili zaidi ya ahadi ya Japan wakati wa mkutano wa TICAD mwaka 2016.

Lakini wachambuzi wamesema Japan haina uwezekano wa kuipiku ahadi ya China katika mkutano wa mwaka huu, unaoanza kesho na kumalizika Ijumaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles