23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu mkuu UN aonya hali mbaya ya mazingira

Biarritz, ufaransa

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, amesema dunia inakabiliwa na hali ya dharura ya mazingira.

Aliwataka viongozi katika mkutano wa Septemba 23 mjini New York, Marekani kufikia makubaliano ya kupunguza gesi zinazoharibu mazingira kwa zaidi ya kile kilichoahidiwa katika makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 kuhusu hali ya hewa.

Guterres aliyasema hayo jana katika mkutano wa kundi la mataifa yenye viwanda mjini Biarritz nchini Ufaransa.

Aliongeza kwamba ulimwengu uko katika hali mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa katika mkutano wa Paris, kwa hiyo ni muhimu nchi zikadhamiria kuongeza kile kilichoahidiwa mjini Paris.

Guterres alisema eneo la theluji la Greenland linayeyuka kwa kiasi kubwa na kwamba mwaka 2015 hadi 2019 ilikuwa miaka mitano yenye joto kali katika rekodi za dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles