Christopher Msekena
OBADEAR Mnyanduli, mwimbaji wa Injili nchini anayefanya vizuri jijini Dodoma, ameweka wazi kuwa mapokezi ya wimbo wake Mwanadamu ni Mwanadamu umepokewa vyema kutokana na ujumbe wake.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mnyanduli alisema wimbo huo umebeba jina la albamu yake mpya huku ujumbe aliouimba ndani ukiwa umebeba ushuhuda wa maisha yake wakati anaanza muziki.
“Mwanadani ni Mwanadamu umewagusa wengi ndiyo maana umepokewa vizuri, kiukweli wakati naanza hii huduma binadamu walikikatisha tamaa, wakanitengenezea vikwazo vingi ili nisifanikiwe lakini Mungu aliniwezesha nikafanikiwa hadi kufikia hapa,” alisema Mnyanduli.