Wema asaidia watoto yatima

0
1320

Brighiter Masaki, Dar es salaam

MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu, ametoa msaada wa nguo na mahitaji mengine kwa watoto yatima kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Miongoni mwa nguo ambazo amezitoa ni zile ambazo alikuwa anazivaa yeye mwenyewe akiwa na mwili mkubwa, hivyo aliamua kuzipunguza kwa ajili ya watoto hao.

“Kuna baadhi za nguo zangu zilikua hazinikai tena baada ya mwili kupungua, hivyo nikaona bora ya kuzipeleka kwa fundi na kuzipunguza kwa ajili ya watoto.

“Mbali na kuwapa nguo pia kulikuwa na mahitaji mengine mbalimbali ambayo nimetoa kwa ajili yao,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here