32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Frida wa BSS: Mazingira yanakwamisha wasichana kushindana

FRIDA AMANI BSSMSHINDI wa tatu katika shindano la Bongo Star Search (BSS) 2015, Frida Aman, amesema mazingira magumu na tamaduni kandamizi ndizo zinazochangia kumkandamiza msichana hasiweze kushindana na wanaume katika kila jambo ikiwemo muziki.

Alisema anaamini mazingira wanayopitia wasichana yangekuwa yanapitiwa na wavulana hali za ushindani zingekuwa sawa, lakini wasichana wengi wanaonekana kushindwa kwenda na kasi ya wavulana kwa kuwa tu mazingira yao yanatofautiana sana.

“Mimi naweza kutaka kujifunza muziki muda fulani nikashindwa kwa kuwa nina kazi za kuosha vyombo, kupika kuandaa chakula na mambo mengine yanayoaminika hufanywa na wasichana lakini mtoto wa kiume akapata muda wa kutosha wa kujifunza kuimba hivyo hatuwezi kuwa sawa wao wanapata muda mwingi wa kufanya mambo tofauti na sisi wa kike,’’ alieleza Farida.

Farida ambaye alipata zawadi ya milioni tano baada ya kushika nafasi hiyo, anasema licha ya kuwa chini ya uongozi wa Tip Top Connection, lakini pia malengo yake ni kufikia ngazi kubwa katika muziki anaoufanya ili umsaidie yeye na familia yake kwa miaka ijayo.

“Nina malengo mengi lakini kubwa ni kutokuacha sanaa kwa kuwa naipenda na naamini miaka ijayo nitakuwa msanii mwenye jina na mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi,’’ alisema.

Frida ni msanii wa muziki wa hip hop, pia ni mwanafunzi na dj aliwahi kutangaza Redio 5 ya Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles