25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

JKT yatoa ujuzi wa namna bora ya kufuga samaki

Hadija Omary, Lindi

Katika kutekeleza kauli mbiu ya maonyesho ya wakulima Nane nane  2019 inayosema “kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi, Jeshi la kujenga Taifa (JKT), limeamua kuunga mkono kaulimbiu hiyo kwa kuwafundisha wananchi wa kanda ya kusini njia bora ya Kufuga samaki wengi aina ya Sato katika eneo hilo.

Akizungumza na Mtanzania Digital mtaalam wa kufuga samaki, lusekelo Anengisye, katika banda lao la maonyesho ya nanenane kanda ya kusini Ngogo amesema njia ya kufuga Samaki kwa kutumia matanki ni rahisi na kunawafaa zaidi watu ambao wamekuwa na changamoto ya maeneo ya kufugia.

Amesema wananchi walio wengi wanaoishi mijini wameonekana wanashindwa kufuga samaki kutokana na changamoto ya uchache wa maeneo waliyonayo  hivyo kuwafanya wasione umuhimu wa zoezi hilo.

“Mfano katika ufugaji wetu wa kawaida katika mita  moja tunaweza kufuga samaki kuanzia nane mpaka watano, lakini kwa kutumia njia hii kwa mita moja hiyo hiyo  tunafuga samaki 40 mpaka 50 kwa kuwaongezea mfumo  rafiki wa hewa unaowawezesha samaki kupumua vizuri.

Kwa upande wake Meneja wa banda la JKT maonyesho ya Nanenane kanda ya kusini Ngongo Lindi,  Charles Aloyce, amesema kuwa pamoja na kuwafundisha wananchi namna ya kufuga samaki katika eneo dogo lakini pia Jeshi hilo linawafundisha wananchi  njia rahisi ya kutotolesha vifaranga vya samaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles