30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaja na mpango wa kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo

Lulu Mussa, Tarime

Serikali imeandaa mpango kazi wa taifa wa kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao umeainisha fursa mbalimbali zitakazowezesha sekta ya wachimbaji wadogo kuendelea na shughuli za uzalishaji wa dhahabu bila kuathiri mazingira.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara hususani maeneo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko ya dhahabu kupitia masoko ya madini ya mikoa yanayojengwa katika mikoa yote nchini, upatikanaji wa mikopo midogo na ya kati kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu na kuwezesha vikundi vya kinamama wanaojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu kwa kutoa mafunzo kuhusu uchenjuaji salama na rafiki kwa mazingira na mikopo.

Sima amesema ofisi yake inaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu kuhusu madhara ya zebaki kwa afya ya binadamu na mazingira na kuwataka wachimbaji wadogo kuchenjua dhahabu kupitia vituo mahiri saba vya mafunzo na uchenjuaji wa dhahabu vinavyojengwa katika mikoa ya Simiyu, Mara, Kagera, Katavi, Mbeya, Ruvuma and Tanga na Geita chini ya Wizara ya Madini.

“Serikali imeona umuhimu wa kuungana na jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi ya zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo na kuwaelimisha kutumia katika njia salama na rafiki wa mazingira,” amesema.

Sima amesema fursa ya kujionea shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki ambayo imebainika kuwa na athari kwa afya za binadamu na mazingira kwa ujumla.

“Zebaki inasababisha magonjwa ya ngozi, moyo, figo na kuharibu mfumo wa neva za fahamu endapo watumiaji hawatazingatia miongozo iliyopo.

“Sisi kama serikali lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunawaelimisha wananchi wetu kwa kuwaambia madhara ya matumizi ya zebaki na kuwashawishi kutotumia zebaki kwa shughuli za uchenjuaji dhahabu Sima alisisitiza,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles