27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kenyatta awataka viongozi kumui Laboso

Nairobi-Kenya

RAIS Uhuru Kenyatta, amewataka viongozi wa siasa kuiga mfano wa marehemu Gavana wa Bomet, Joyce Laboso ambaye alimtaja kama kiongozi mtumishi.

Rais alisema  hayo, mwishoni kwa wiki wakati wa mazishi ya Laboso, kuwa alitumikia familia yake, wapigakura wake na Wakenya kwa roho ya kujitolea na akafanikiwa kwa njia ambayo ilionekana wazi.

“Alikuwa mkarimu na aliyejitolea kuwasaidia watu wa Sotik, Bomet na Wakenya kwa ujumla. “Hakuwa mtu mwenye majivuno,bali mnyenyekevu,ndiyo maana alipendwa na watu wote. Alitangamana na watu wote kwa furaha. Nyote hapa mwafaa kuiga mfano wa kiongozi huyu tunayempumzisha,” amesema Rais Kenyatta

Katika maisha yake ya kisiasa, marehemu Laboso, Rais Kenyatta alisema, alihudumu kama Mbunge wa Sotik kwa mihula miwili, Naibu Spika na Gavana wa Bomet.

 “Marehemu Laboso ni kiongozi ambaye hakuonyesha uchu wa kutumia vibaya afisi yake kwa kujilimbikizia mali bali mtumishi wa wananchi aliyefanya hivyo kwa uadilifu,” kiongozi wa nchi amesisitiza.

Kiongozi wengi, waliimminia sifa mume wake Laboso, Dk. Edwin Abonyo, kwa kuunda familia yenye mshikamano, licha ya wawili hao kutoka jamii mbili zenye mila, tamaduni na imani tofauti.

“Nakupongeza Dk. Abonyo kwa kupuuzilia mbali baadhi ya mila na tamaduni zilizopitwa na wakati na kujenga familia thabiti na ya kupigiwa mfano,” alisema Rais Kenyatta.

Ibada hiyo, ilifanyika  Shule ya Upili ya Kandege na kuhudhuriwa na Naibu Rais, William Ruto, aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, waliokuwa makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi miongoni mwa viongozi wengine

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles