23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yamwekea vikwazo waziri mambo nje wa Iran

TEHRAN, IRAN

MAREKANI imemuwekea vikwazo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif, katika hatua isiyokuwa ya kawaida.

Uamuzi huo wa Marekani unatajwa kufunga njia zote za kidiplomasia wakati tayari kukiwa na mvutano mkubwa kati ya nchi hizo mbili. 

Wizara ya Fedha ya Marekani imesema imemuwekea vikwazo Zarif kwa sababu anafanya maamuzi kwa niaba ya kiongozi wa juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Ali Khamenei. Zarif, ambaye ni mwanadiplomasia aliyesomea Marekani, amekuwa mjumbe mkuu wa Iran kwenye jukwaa la kimataifa na mtu muhimu wa mawasiliano kuhusu sekta ya nchi hiyo ya nishati ya nyuklia kwa ajili ya matumizi ya kiraia, ambayo Marekani inasema inatumika kisiri kuuficha mpango wa kutengeneza silaha. 

Vikwazo vya Marekani vinazuia mali zozote za Zarif nchini Marekani na kuzuia taasisi za Marekani kufanya biashara naye.

Hata hivyo Waziri huyo amepuuzilia mbali vikwazo hivyo alivyowekewa akisema havitamuathiri pamoja na familia yake kwa sababu hana mali zozote wala maslahi yoyote nje ya Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles