24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mgonjwa mwingine augua Ebola

GOMA, CONGO

MAOFISA nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo wametangaza  kuanza kutoa chanjo dhidi ya Ebola wakati ambapo mgongwa mwingine amethibitika kuugua ugonjwa huo mjini Goma Mashariki.

Hofu kubwa imetanda kwa mara nyingine mjini Goma mashariki mwa Congo baada ya kutangazwa kuwepo kwa mgonjwa wa pili wa homa ya Ebola.

Madaktari wamesema mgonjwa huyo mpya wa Ebola alingia mjini Goma akitokea jimbo la Ituri wiki mbili zilizopita.

Inaelezwa kuwa mtu huyo alitengwa baada tu ya kuonesha dalili zote za homa hatari ya Ebola na kupelekwa kwenye eneo maalumu ili kupewa matibabu. 

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Goma, kiongozi wa kikosi kinachopambana na Ebola mkoani Kivu Kaskazini na Ituri, Jack Muyembe alisema mikakati imechukuliwa ili mgonjwa huyo apatiwe matibabu mjini Goma.

Ofisa huyo aliyeteuliwa na rais Tshisekedi baada ya kujiuzulu uwaziri wa afya alisema operesheni ya chanjo itaanzishwa mjini Goma kwa lengo la kuzuia maambukizi mapya kwa wakaazi wanaoonekana kuishi katika wasiwasi.

Kisa hiki ni cha pili kugunduliwa ndani ya mwezi mmoja baada ya mchungaji wa kanisa la Protestanti kufariki kutokana na ugonjwa huo wa Ebola wakati alipokuwa akirejeshwa mjini Butembo. 

Ripoti ya wiki kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO)  imebainisha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na Ebola imefikia 1803 na watu 770 wamepata ahueni tangu mwezi wa Agosti mwaka jana.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya WHO kutangaza kwamba homa ya Ebola ni janga la kimataifa na kutaka uungwaji mkono wa mataifa yote ili kukabiliana na ungonjwa huo hatari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles