FLORENCE SANAWA-MTWARA
Madiwani wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, wamewaomba wabunge kuwasaidia kupata gari la wagonjwa ili kuweza kukabiliana na changamoto inayowakabili ya kusafirisha wagonjwa.
Akitoa ombi hilo katika kikao cha baraza la madiwani la manispaa hiyo Naibu Meya, Shadida Ndile (CCM), amesema wabunge hao wakishirikiana wanaweza kutatua tatizo hilo ambalo kwa sasa limekuwa kubwa.
Amesema kuwa endapo manispaa hiyo ikipata gari la wagonjwa itasaidia kutatua changamoto ya usafiri kwa wagonjwa inayowakabili kwa Muda mrefu.
“Kwakweli manispaa yetu haina gari la kubebea wagonjwa hivyo tupambane kwa umoja wetu ili manispaa yetu iweze kupata gari hiyo itakayotusaidia kupunguza changamoto tuliyonayo hasa tunapopata mgonjwa anaetakiwa kuwahishwa kwenye matibabu” amesema Ndile.