27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: hatutaruhusu kilichotokea kwenye pamba kijirudie tena

Derick Milton – Simiyu

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema kuwa serikali haitakubali tena changamoto zilizojitokeza kwenye zao la pamba msimu huu kujirudia katika msimu ujazo wa zao hilo.

Bashe ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Julai 31, baada ya kutembelea chama cha msingi cha ushirika (Amcos) Zuya,  kilichopo kata ya Nyakabindi halmashuari ya Mji wa Bariadi kabla ya kwenda kwenye viwanja vya nanenane kukagua maandalizi ya sherehe hizo kitaifa.

Kauli ya Bashe imetokana na kuendelea kuwepo kwa pamba nyingi iliyohifadhiwa kwenye maghala ya vyama vya msingi vya ushirika na kwa wakulima bila ya kununuliwa huku tatizo kubwa likielezwa kuwa bei kwenye soko la dunia.

Amesema kuwa serikali na bodi ya pamba nchini wamejifunza kupitia changamoto hii, na tayari wameanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo cha zao hilo kuhakikisha haliwezi kujirudia tena.

“Tukiwa kama serikali hatutaruhusu tena hali hii ijitokeze kwasababu tutamfanya mkulima huyu wa pamba akate tamaa kulima zao hili, hatutaruhusu tena lijitokeze na tayari tumeanza mkakati wa kuhakikisha hilo,” amesema.

Amesema kuwa benki kuu ipo katika hatua za mwisho za kuhakikisha wafanyabishara wote wanapatiwa pesa na ijumaa ya wiki hii taratibu zote zitakuwa zimekamilika kwa ajili ya kuanza kununua pamba iliyoko kwa wakulima.

“Benki kuu wapo katika hatua za mwisho za kuhakikisha wanaruhusu benki kutokopesha wanunuzi wa pamba ili waweze kununua pamba yote iliyoko kwa wakulima, na taratibu hizo hadi kufika ijumaa zitakuwa zimekamilika” amesema Bashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles