33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Puma kuendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi

Mwandishi Wetu

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imesema itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi mbalimbali ikiwa ni mkakati wake wa kupunguza ajali nchini.

Pia kampuni hiyo imetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa zaidi ya wanafunzi 4500 katika shule tano za msingi Jijini Dodoma huku ikiahidi kuendelea kutoa elimu hiyo na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa mabalozi kwa wengine.

Akizungumza leo julai 25 jijini Dodoma mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana,  Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah, amesema programu hiyo ya mwezi mmoja kwa jiji hilo ilihusisha mafunzo ya usalama barabarani kwa walimu 15 na wanafunzi 4500, katika shule tano

“Puma Energy Tanzania imeamua kuja jijini Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa haraka wa jiji hili ambapo shughuli za kijamii na ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto wanapokwenda shuleni na kurudi nyumbani,” amesema.

Dhahana amebainisha lengo ni kuwafanya watoto kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara ili kuongeza uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa Watanzania.

“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima. Puma Energy Tanzania itaendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya watanzania,” amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amesema Puma Energy Tanzania ni kampuni iliyoamua kutoa elimu ya usalama barabara nchini huku akitoa ombi kwa kampuni hiyo kufundisha walimu ili wakifundisha masomo ya kawaida wawe pia wanataka na elimu ya usalama.

“Nimesikia ombi la walimu na wanafunzi la kuhitaji alama za barabarani, hivyo Serikali itaendelea kuweka alama hizo pia nimezungumza na wenzetu wa Puma wamekubali kupaka rangi za usalama barabarani na wataanza na shule tano ambazo zimepatiwa elimu hii ya usalama  barabarani,”amesema Mavunde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles