26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Masauni: Ni aibu kutorosha nyara za serikali

Asha Bani – Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni, amesema ni aibu kusikia mali ikiwemo nyara za serikali na madini zinatoroshwa na kukamatiwa nchi za jirani kutokana na kutokuwa na ulinzi wa kutosha.

Masauni ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 25, mara baada ya kuanza ziara ya kukagua usalama wa viwanja vya ndege ambapo amepoanza na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua ya Rais John Magufuli imewashtua na kuona kuna haja ya kufanya kazi kwa muunganiko mkubwa kati ya Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mapato TRA pamoja na wafanyakazi wa viwanja vya ndege ili kuhakikisha kunakuwa na usalama.

“Nimekagua kwa kuanza na huu uwanja mkubwa na nitaendelea katika viwanja vingine lengo kuhakilisha naangalia maeneo ya usalama na hakuna mtu kupitisha dawa za kulevya, nyara za serikali na vitu vingine visivyo halali,” amesema Masauni.

Aidha amesema wataongeza kikosi cha Askari wa kutosha na wenye sifa sambamba na Askari mbwa watakaotumika kukagua mizigo na kubaini vitu vingine ambavyo si halalali ikiwemo dawa za kulevya na kuwakamata wahusika.

Naye Kamanda polisi wa viwanja vya ndege (ACP), Jeremia Shila, amesema hatasita kumchukulia hatua yeyote askari atakayegeuka na kufanya kazi kinyume na maadili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles