31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Tunisia afariki dunia

Tunisia

Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi amefariki dunia leo Alhamisi Julai 25, katika hospitali  ya  kijeshi mjini  Tunis akiwa na umri wa miaka 92, baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.

Taarifa zinasema Essebsi alipelekwa  hospitalini hapo jana jioni kwa  mara ya pili  ndani ya mwezi mmoja.

Rais huyo alikuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani baada ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza na amekuwa  madarakani  tangu  mwishoni mwa mwaka 2014 baada ya kusinda uchaguzi huru wa kwanza kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu.

Mapema mwaka huu, Essebsi alitangaza kwamba hatogombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba mwaka huu alisema kwamba muda umewadia kwa kijana kushika nafasi hiyo ya uongozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles