27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

NSSF kusaka waajiri binafsi

Nora Damian

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuanzia wiki ijayo utaanza kufanya ukaguzi nchi nzima kusaka waajiri ambao wanachama wao hawajaandikishwa. 

Kulingana na mabadiliko ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii yaliyofanywa mwaka jana, wanachama wa mfuko huo kwa sasa ni wale walio katika sekta binafsi na isiyo rasmi.

Akizungumza leo Julai 25, kuhusu kampeni ya NSSF na Marafiki, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, amesema tayari wanayo orodha ya waajiri wote nchi nzima hivyo watapita kila ofisi.

“Watu wote walio katika sekta binafsi na hata kampuni ambazo Serikali ina hisa lakini hazizidi asilimia 30 wanatakiwa waandikishe wanachama wao NSSF,” amesema Erio.

Kuhusu kampeni ya NSSF na Marafiki amesema inalenga kujenga undugu na wanachama na kuhakikisha wanapata huduma bora kwa faida ya maisha ya sasa na ya baadaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,406FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles