29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Madrid wamjia juu Eden Hazard

MADRID, HISPANIA

MASHABIKI wa Real Madrid, wamemjia juu mshambuliaji wao mpya Eden Hazard baada ya kuonekana mazoezini akiwa na simu yenye kasha la picha ya watoto wake wakiwa wamevaa jezi za Chelsea.

Hazard amejiunga na Real Madrid wakati huu wa kiangazi akitokea Chelsea kwa kuweka rekodi ya usajili wa kitita cha pauni milioni 150 na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka England kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Mchezaji huyo raia wa nchini Ubelgiji aliondoka kwenye viwanja vya Stamford Bridge baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka saba na kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye mashabiki wengi ndani ya kikosi hicho.

Hazard mwenye umri wa miaka 28, aliweka wazi kuwa anaipenda sana Chelsea kabla ya kuondoka, lakini kutokana na kiasi kikubwa che fedha alichowekewa kutoka Madrid, hakuweza kukataa.

Mchezaji huyo kwa sasa anajiandaa na maisha mapya ndani ya Real Madrid, lakini kabla wachezaji wa timu hiyo hawajapanda ndege kuelekea Kaskazini mwa Marekani kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi Hazard alionekana akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Montreal akiwa ameshika simu mkononi ambayo kasha lake lina picha ya watoto wake watatu wakiwa wamevaa jezi za Chelsea.

Picha hiyo ya Hazard imesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wa Chelsea wakifurahia huku wengi wao wakidai mchezaji huyo bado atabaki kuwa na chembe chembe za Chelsea, hivyo atabaki kuwa Blue.

Wengine wamedai kuwa Hazard bado anaipenda Chelsea, hivyo amekwenda Real Madrid kwa ajili ya kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo tangu akiwa mdogo.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa Real Madrid wamemtaka mchezaji huyo abadilishe aina hiyo ya kasha la simu ili kutuliza roho za mashabiki.

Katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi, Real Madrid wanatarajia kucheza mchezo wa ICC Julai 20 dhidi ya Bayern Munich.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles