Vyombo vya habari vyatakiwa kuupa kipaumbele mkutano wa SADC

0
615
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas

Nora Damian

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuupa kipaumbele mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi ujao.

Kwa mara ya mwisho mkutano huo ulifanyika 2003 chini ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na katika mkutano wa mwaka huu Rais Dk. John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza leo Julai 13 wakati wa kufunga mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu SADC, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas, amesema kuna mambo mengi kuhusu jumuiya hiyo ambayo Watanzania wengi hawayafahamu hivyo ni nafasi ya vyombo vya habari kuwafahamisha.

“Mkutano huu ni mkubwa sana, mara ya mwisho ulifanyika nchini mwaka 2003 na sasa tumepata tena fursa hii, hili ni tukio letu tulibebe wote.

“Hoja siyo tu Tanzania inakwenda kuwa mwenyeji lakini kuna mambo mengi yanachanganya na kukanganya, tuwasaidie Watanzania kuelewa mengi kuhusu SADC,” amesema Dk. Abbas.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here