25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Wanawake waliochomewa maboma Babati waomba msaada kwa wadau

JANETH MUSHI-BABATI

Wanawake wa jamii ya Kifugaji wa kabila la Watatoga, waliochomewa maboma yao katika Kijiji cha Vilima vitatu, Babati vijijini Mkoani Manyara, wameomba wadau kuwanusuru watoto wadogo ambao hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu kwa kulala nje huku kukiwa na baridi kali.

Katika kijiji hicho zaidi ya maboma 30 ya wananchi hao yameteketezwa kwa moto kwa madai kuwa wananchi hao wamejenga nyumba eneo la shoroba za wanyama katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori(WMA) ya Burunge.

Wakizungumza kijijini hapo katika mkutano wa hadhara baadhi ya wanawake hao walidai kuwa wamekuwa wakiteseka kwa kulala nje kuanzia jumatatu Julai 9, huku watoto wadogo wakishindwa kuhimili mazingira hayo kutokana na baridi kali.

“Watoto wetu wanaishi katika mazingira magumu baada ya kuchomwa kwa maboma, hakuna neti huku nje usiku kuna mbu sana hatuna hata maturubali ya kulala,baridi ni kali tunalala njaa wakati mwingine hivyo tunaomba walau msaada wa maturubali tulaze hata watoto ndani wasipigwe na na baridi,”amesema Dorkas Babayi, mmoja wa wanawake hao

“Tunaomba wadau watusaidie wafugaji wanawake na wakati mwingine tunakosa maziwa ya kutosha ya kuwapa watoto kwa sababu ndama wanalala na mama zao kwa sababu hakuna mahali pa kuwalaza kwa hiyo tunakosa maziwa,”

Naye Gidamushoto Murisha aliomba wafugaji hao wapewe ruhusa walau kuweza kunywesha maji mifugo yao baada ya kukatazwa kunywesha mifugo katika Mto Heri ambao huutumia siku zote kunyweshea mifugo hiyo.

“Tatizo lingine linalotusumbua ni kuhusu mifugo yetu ambayo haijanywa maji kuanzia jumatatu tunaomba turuhusiwe kwenda kunywesha maji kwani watakufa kwa kukosa maji,haturuhusiwi kukanyaga ile ng’ambo kule wala kunywesha mifugo kule,”alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Belela Erasto, amesema katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kuhusu wananchi hao walikubaliana na Ofisa Wanyamapori na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi, walifika katika eneo hilo na kuhakiki maboma na kukubaliana watu hao wabaki katika eneo hilo kwani mpango uliwakuta na kuomba kutatuliwa mgogoro huo haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles