22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Beyonce alivyoipa heshima lugha ya Kiswahili

SWAGGAZ RIPOTA

KAMPUNI kongwe ya uandaaji filamu nchini Marekani, Disney ,inatarajia kufyatua sinema yake mpya, The Lion King, Julai 19 mwaka huu kwenye majumba ya filamu baada ya Jumatano wiki hii kuzinduliwa huko Hollywood.


Gumzo kubwa ni hatua ya staa wa muziki, Beyonce Knowles Carter, kutumia maneno ya lugha ya Kiswahili katika wimbo wake Spirit ambao upo kama ‘soundtrack’ kwenye filamu hiyo.

Mwanzoni kabisa mwa ngoma hiyo yenye dakika 4:37, yanasikika maneno ya Kiswahili sanifu yakisema: ‘Uishi kwa muda mrefu mfalme
(Uishi kwa uishi kwa)
Uishi kwa muda mrefu mfalme
(Uishi kwa, uishi kwa),” kisha Queen B, anaendelea kuimba Kingereza.

Unaweza kuona ni jinsi gani lugha ya Kiswahili inakua kwa kasi na imekuwa na nafasi kubwa kwenye sanaa ulimwenguni kote kiasi cha kutokuwa ajabu tena kuisikia kwenye filamu na nyimbo za wasanii wakubwa.


Ukiacha hili la Beyonce, miaka kadhaa nyuma hata Michael Jackson kwenye Liberian Girl, Omario, Nas na wengino waliwahi kuimba Kiswahili katika ngoma zao, hivyo inatupa tafsiri kuwa tunahitaji kuwekeza zaidi kwenye lugha hii.

Inatarajiwa kusikia maneno mengi ya Kiswahili yakitumika katika filamu ya The Lion King maana ndani yake kuna mhusika mmoja anaitwa Simba, jina la Kiswahili la mnyama ila jambo la ajabu utaona aliyeingiza sauti yenye maneno ya Kiswahili kwenye wimbo, Spirit siyo Mtanzania wakati Bongo tuna wataalamu wa lugha hii tamu.

Disney, wanasema wimbo huo unapatikana kwenye albamu ambayo imeandaliwa na Beyonce mwenyewe kama ‘soundtrack’ ya filamu ya The Lion King, ambayo imebeba kisa kisa cha simba mdogo anayetafuta namna ya kuwa mfalme na kuigizwa na mastaa wengi akiwamo Beyonce, Chaldish Gambino, Seth Rogen, Chiwetel Ejiofor, Billy Eichner na Keegan Michael.

Intro
Uishi kwa muda mrefu mfalme
(Uishi kwa uishi kwa)
Uishi kwa muda mrefu mfalme
(Uishi kwa, uishi kwa)
Verse
Yeah, yeah, and the wind is talkin’
Yeah, yeah, for the very first time
With a melody that pulls you towards it
Paintin’ pictures of paradise
Chorus
Sayin’ rise up
To the light in the sky, yeah
Watch the light lift your heart up
Burn your flame through the night, woah
Chorus
Spirit, watch the heavens open (Open)
Yeah
Spirit, can you hear it callin’? (Callin’)
Yeah
Verse
Yeah, yeah, and the water’s crashin’
Trying to keep your head up high
While you’re trembling, that’s when the magic happens
And the stars gather by, by your side
Chorus
Sayin’ rise up
To the light in the sky, yeah
Let the light lift your heart up
Burn your flame through the night, yeah
Chorus
Spirit, watch the heavens open (Open)
Yeah
Spirit, can you hear it callin’? (Callin’)
Yeah

Chorus
Your destiny is comin’ close
Stand up and fi-i-ight

Bridge
So go into that far off land
And be one with the Great I Am, I Am
A boy becomes a man, woah

Chorus
Spirit, watch the heavens open (Open)
Yeah
Spirit, can you hear it callin’? (Callin’)
Yeah
Spirit, yeah, watch the heavens open, open
Yeah
Spirit, spirit, can you hear it callin’? (Callin’)
Yeah
Outro
So go into a far off land.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles