27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kamwelwe: Hatujazuia mizigo kupelekwa bandari kavu

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, amesema Serikali haijazuia makontena kwenda bandari kavu (ICD’S), bali taarifa zilizokuwa zikidai imezuia zililenga kuchafua biashara ya Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema kilichofanyika ni marekebisho ya sheria ambayo inatamka anayeamua kontena liende wapi ni mteja kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na si vinginevyo.

Kamwelwe alisema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa madini kutoka nchi mbalimbali, ambao walitoa changamoto zinazowakabili.

 “Lakini na wao inabidi tuwafahamishe maana tunaharibiwa biashara na maneno, juzi hapa tulirekebisha sheria, kwamba sasa atakayeelekeza kontena liende wapi ni TPA.

“Lakini ikabadilishwa ikawa eti nimezuia makontena yasiende bandari kavu, anayezuia makontena yasiende bandari kavu ni mamlaka kwa kushirikiana na mwenye mzigo.

“Kauli ya kusema kwamba Tanzania imezuia makontena yasiende bandari kavu ni uongo, tena uongo wa mchana. Tulichoondoa ni kitendo cha mwenye meli kusema mzigo uende ICD, amejuaje ICDs zetu, hiyo ndiyo tumeitoa,” alisema.

Kamwelwe alisema katika kuhakikisha Serikali inaongeza biashara Bandari ya Dar es Salaam, aliamua kuwaalika wachimba madini wakubwa duniani kwa sababu Serikali imetoa fedha nyingi kukarabati bandari, reli na barabara.

“Tuliwaita ili kujua changamoto zao ni nini, malengo yetu tunataka mzigo upite asilimia 100 kwenye Bandari ya Dar es Salaam, wao wamesema wanapitisha asilimia 20 hadi 40.

“Wamebainisha changamoto zao na ukiangalia ni za kiutendaji, lakini nimewajibu kwamba huko zamani TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) ilikuwa peke yake, bandari peke yake, Tazara (Reli ya Tanzania na Zambia) peke yake na reli ya kati peke yake.

“Sasa hivi wote tutakaa kwenye jengo moja ili kuharakisha  mzigo upite, ndiyo maana wamesema dhahabu ina gharama kubwa na wao wana mikataba na makampuni China wanasema mzigo mkubwa unakwenda China, kiwanda cha China pengine kinataka tani 500,000 kwa mwezi, kwa hiyo lazima ipite,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles