28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Unene unasabisha saratani kuliko uvutaji sigara

LONDON-UINGEREZA

UNENE sasa umetajwa kuwa moja ya kisababishi cha ugonjwa wa saratani nchini Uingereza kuliko uvutaji sigara.

Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani imesema, saratani ya ini, utumbo, ovari zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uzito mkubwa kuliko kuvuta tumbaku.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo, mamilioni ya watu duniani wako hatarini kuugua saratani kwasababu ya uzito.

Kwamba watu wenye uzito mkubwa  wanaogua saratani huzidi idadi ya wavuta sigara kwa wastani wa watu wawili kwa mmoja.

Taasisi hiyo imesema pamoja na taarifa hiyo haimaanishi kwamba uvutaji sigara ni salama bali vyote viwili vinahatarisha afya.

Takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo zinaonyesha kuwa uzito mkubwa au unene husababisha wagonjwa wa saratani 22,800 kila mwaka, ukilinganisha na uvutaji wa sigara unaosababisha watu 54,300 kuugua saratani.

Imeeleza kuwa  wakati idadi ya wavuta sigara ikipungua, idadi ya watu wenye uzito mkubwa inaongezeka na hivyo kushauri suala hilo kushughulikiwa.

Wakati taasisi hiyo ikibainisha uhusiano kati ya uzito na saratani lakini bado kibailojia suala hilo halijaeleweka vyema.

Katika kuweka sawasawa hilo, taasisi hiyo imesema kuwa na uzito mkubwa au unene haimaanishi ni lazima mtu huyo apate saratani bali anaongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa watafiti saratani mbalimbali zinahusishwa na uzito mkubwa ni pamoja na ya matiti kwa wanawake waliokoma hedhi (menopause), utumbo, ini.

Nyingine ni saratani ya damu, saratani ya ubongo, koo, tezi, figo, kongosho, tumbo na ovari.

Taasisi hiyo pia imesema uhusian kati ya unene na saratani ni kwa watu wazima pekee, ingawa imeshauri kwa upande wa watoto wadogo ni muhimu kuwa kwenye tahadhari.

Taasisi hiyo imekuja na taarifa hiyo ikiwa ni wiki kadhaa tu tangu Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, nchini Dk. Faustine Ndugulile kueleza hofu ya ongezeko la watu wenye uzito mkubwa.

Dk. Ndugulile ambaye alikuwa akijibu swali bungeni lililoulizwa bungeni na mbunge Zainabu Mwamwindi aliyehoji tatizo la utapiamlo,  alisema zaidi ya asilimia kumi ya watanzania wanasumbuliwa na tatizo hilo la uzito wa kupindukia.

Aidha aliaunisha kuwa tatizo la uzito uliopindukia ni kubwa kwa wanaume na wanawake wa maeneo ya mjini kuliko vijijini.

Akizungumzia kuhusu utapiamlo Dk. Ndugulile alisema miongoni mwa jitihada ambazo zimechukuliwa na serikali ni pamoja na kuwa na mpango wa kazi wa lishe kwa kuangalia vipaumbele katika maeneo sita.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na watoto wachanga, wajawazito, lishe ya watu wazima na kuangalia usimamizi wa upatikanaji wa chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles