Derick Milton, Simiyu
Tamasha kubwa la michezo katika mkoa wa Simiyu ambalo hufanyika kila mwaka na kushirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka mikoa ya kanda ya ziwa (Simiyu Jambo Festival), limefanyika leo Mjini Bariadi huku mikoa ya shinyanga na Mwanza iking’ara.
Mikoa hiyo imefanya vizuri katika michezo ya mbio za baiskeli kwa wanawake, wanaume, pamoja na walemavu, huku mwenyeji Simiyu na Mkoa wa Mara wakishika nafasi za chini.
Katika mbio za baiskeli kilimota 150 kwa wanaume, mshindi wa kwanza hadi wa tatu wametoka mkoa wa Shinyanga, na mshindi wa nne na watano wakitoka katika mkoa mwenyeji Simiyu.
Kwenye mbio hizo za baiskeli kilometa 80 wanawake, mshindi wa kwanza alitoka mkoa wa Mwanza, huku mshindi wa pili hadi wa tatu wakitoka Mkoa wa Shinyanga na walemavu mshindi wa kwanza hadi wa watatu wakitoka Mwanza.
Akifunga tamasha hilo Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, amesema kuwa tamasha hilo limelenga kukuza sekta ya michezo katika mkoa huo, ikiwa pamoja na kuibua vipaji kwa ajili ya kushiriki kimataifa.
Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA), pamoja na Kampuni ya Jambo, likibeba ujumbe wa kupiga vita mimba na ndoa za utotoni.