24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Timu 20 kuchuana Ndondo Cup Arusha

 Janeth Mushi, Arusha

Mashindano ya  Jumuiya  ya Michezo  jijini  Arusha  maarufu Arusha Ndondo Cup yamefunguliwa rasmi katika viwanja vya Jeshi kikosi cha 977 Tanganyika Packers Moshono, ambapo jumla ya timu 20 zitachuana.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, leo Juni 30, Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Tan Communication Media,  wamiliki wa Redio 5 Arusha, Ashura Mohamed amewataka vijana watakaoshiriki mashindano hayo kuyachukulia kama chachu ya kuendeleza vipaji vyao.

Amesema mchezo wa soka hapa nchini na duniani ni mchezo unaoongioza kuwa na washabiki wengi hivyo waendelee kufanya mazoezi kwa bidii  na kuwa na nidhamu  ili kukuza vipaji na kutumia  mashindano  hayo  vyema kujitangaza.

Ashura amewataka marefa ambao wanachezesha mechi hizo na waratibu wa mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanatumia sheria 17  za mpira wa miguu ili kuhakikisha kuwa mshindi  anapatikana kihalali.

“Nimeelezwa kuwa mashindano haya yameanza mwaka  2015, yakiwa na timu 12 leo tuna timu 20 ni hatua nzuri na inaonesha wazi kuwa mmejipanga vizuri nisisitize tu sheria za mpira zifuatwe, ” amesema.

Aidha amesema ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo ataongeza zawadi ili kuongeza hamasa kwa timu zitakazoshiriki na kufanya vyema zaidi.

Naye Mratibu wa mashindano hayo ambaye ni mdau wa michezo kutoka wilaya ya Arumeru Benjamini Mathayo, alitaja moja ya changamoto kubwa ni kukosekana kwa vifaa vya kutosha na fedha.

Alisema mashindano hayo yatasaidia kupunguza idadi ya matukio ya kihalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya huku yakienda sambamba na utunzaji wa mazingira ambapo kila jumapili timu zote zitapanda miti katika maeneo  ya wazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles