32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Daladala Kigamboni wataka kuongezewa ruti

Na AVELINE KITOMARY 

-DAR ES SALAAM 

MADEREVA wa daladala na makondakta katika stendi ya Kigamboni –Kibada, wameiomba Serikali iwarefushie ruti zao ili kupunguza msongamano wa magari katika stendi hiyo.

Akizungumza juzi Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Makondakta Kigamboni -Kibada  (CHAMADAKI), Ahmed Said, alisema wanaomba ruti zirefushwe ili mapato yaongezeke na wao wapate wigo wa kutanuka. 

“Tatizo hapa ni ruti kuwa fupi, magari yakitokea hapa Kigamboni yanaishia Tuangoma, magari hayaruhusiwi kwenda maeneo mengine. Tunaomba Serikali kuangalia hili kwani ruti ikirefushwa msongamano wa magari hapa utapungua na pia mapato yataongezeka,” alisema Said.

Alisema ruti wanazoomba zirefushwe ni Kigamboni kwenda Kipara Mpakani, Mwandege, Kisemvule na Mbagala.

“Kama ruti ikirefushwa, pia itasaidia kupunguza kiwango cha nauli kwa abiria kwani wakifika Tuangoma wanapanda tena magari mengine au bajaji kwa Sh 500, hii inaongeza gharama ya nauli,” alisema.

Mmoja wa madereva, Bakari Yusuph, alisema ubovu wa barabara kuanzia eneo la Msikitini hadi Stendi ya Tuangoma inasababisha magari kuharibika mara kwa mara.

“Wakati mwingine tunagombana na mabosi kutokana na springi za magari kuvunjika, hivyo tunatengeneza magari mara kwa mara na tunapoteza fedha nyingi,” alisema Yusuph.

Alisema wanaiomba Serikali iwajengee barabara hiyo kwani mvua ziliponyesha iliharibika zaidi.

“Tunaomba kujengewa barabara ambayo ni kilometa mbili tu, itasaidia magari yetu kuwa salama,” alieleza Yusuph. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles