29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kujenga hospitali ya kisasa Simiyu

DERICK MILTON NA SAMWEL MWANGA, ITILIMA

SERIKALI imeanza ujenzi wa hospitali mpya ya kisasa katika eneo la kijiji cha Nguno katika  Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu kwa lengo la kuwaondolea kero wananchi ya kutembea
umbali mrefu kutafuta huduma za afya.

Akizungumza kwenye ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo uliofanywa wilayani humo baada ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru, Mganga Mfawidhi, Anorld Musiba amesema zoezi hilo litasaidia kupunguza changamoto wanazopitia wananchi hao.


“Mwaka jana vimetokea vifo vya watu watano, mwaka huu mpaka sasa vimetokea vifo vya watu wawili na vyote ni akina mama wajawazito, serikali imeamua kujenga hospitali wilayani hapa ambapo ujenzi wake unaendelea na utakamilika Juni 30, mwaka huu.

“Ujenzi huu utahusisha majengo saba na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5, hadi sasa gharama
zilizotumika ni shilingi bilioni 2.1 sawa na asilimia 81 ya utekelezaji, tunategemea ujenzi huu utasaidia kumaliza vifo vya kina mama wajawazito na tunatarajia hospitali hii itahudumia wananchi zaidi ya 300,000.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge, Mkongea Ali amesema ameridhishwa na ujenzi huo na  ametaka kuongezwa kwa kasi ya ujenzi huo kabla ya mwaka wa fedha 2018/19 kuisha.

 Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo walishukuru serikali kwa kuwaletea hospitali ambapo wameomba kuharakishwa kwa ujenzi wake ili kuanza kupata huduma mapema.

“Tulikuwa tunateseka sana kwenda Bariadi, ukiangalia huku ni vijijini na miundombinu ya barabara ni mibovu tumekuwa tukitumia muda mrefu kupata matibabu,” amesema Janeth Saguda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles