31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Watatu washikiliwa kwa rushwa

CHRISTINA GAULUHANGA ,DAR ES SALAAM

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), inawashikilia watu watatu akiwamo Diwani wa Kata ya Ukonga (Chadema), Jumaa Mwipopo na Ofisa Mtendaji was kata hiyo, Rozalia Silumbe kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh.400,000 kwa mwananchi aliyekuwa anatuhumiwa kufanya uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mei 24 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema, watuhumiwa hao walikamatwa Mei 22, mwaka huu, saa 9 alasiri, Katika ofisi za Kata ya Ukonga.

Amesema watuhumiwa hao walishawishi na kuomba Rushwa ya Sh.400,000 na kupokea Sh.300,000 kutoka kwa mwananchi huyo.

“Watuhumiwa watafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu tuhuma chini ya kifungu Cha 15 (1) (a)Cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007,”amesema Myava.

Myava amesema katika tukio lingine, Takukuru inamshikilia Deogratias Mgasa (43), mkazi wa Tegeta kwa tuhuma za kujifanya Ofisa wa Takukuru.

Amesema Takukuru ilibaini kwamba Mgasa anatumia kitambulisho bandia kinachoonyesha yeye ni Ofisa Takukuru mwenye cheo cha mchunguzi daraja la Kwanza ambacho alikuwa akikitumia katika kufanya utapeli.

Amesema mtuhumiwa huyo alikutwa na kitambulisho hicho chenye jina la Patrick Ushilobo kilichotolewa Januari 2, mwaka 2014 na Taasisi hiyo kilionyesha kama ni Ofisa wao.

Myava amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 23, mwaka huu, saa 10 jioni, kituo cha mafuta cha Big Born, ambapo aliomba Rushwa ya Sh.milioni 20.

Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa pia na bangi misokoto Saba ambapo uchunguzi unaendelea na atafikishwa mahakamani.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alishawahi kufungwa jela miaka mitatu aliomba Rushwa pia ya Sh.milioni 70 na tangu atoke jela ana wiki mbili.

Aidha Takukuru imewatahadhalisha wananchi kuacha kurubuniwa na matapeli na badala yake watoe taarifa mapema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles