Derick Milton – Simiyu
Meneja wa Wakala wa Mejengo ya Serikali (TBA), mkoani Simiyu Mhandisi Loishorwa Naunga amesema kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi majengo mawili ya upasuaji mkubwa mionzi na maabara katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo miezi miwili kabla ya muda wa mkataba wake ambao ni Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Mtanzania leo Mei 23, Naunga mesema kuwa majengo hayo yanayojengwa kwa gharama za sh.Bilioni 3.5 ambapo mpaka sasa wamepokea kiasi cha sh. Bilioni 1.6
“Tunategemea kama serikali itatuletea kiasi cha pesa kilichobaki tuna uhakika kuwa mwezi Agosti tutakamilisha ujenzi mzima kabla ya muda wa mkataba, ” amesema.
Mganga mafawidhi wa hospitali hiyo Dk. Matoke Muyenjwa amesema kuwa kasi ya mkandarasi ni kubwa na wanategemea kukabidhiwa majengo mapema kabla ya muda wa mkataba.
Dk. Muyemjwa amesema kuwa katika jengo la maabara mkandarsi amekamilisha ujenzi huku jengo la mionzi na upasuaji likiwa kwenye hatua za ukamilishwaji wake.